Karatasi ya sanaa
Shughuli za kisanii zinazofanywa na watoto katika Daraja la 1 zinakusudiwa kuwezesha uthamini wao kwa uzuri na mpangilio na kuimarisha ndani mwao ujuzi fulani na uwezo, miongoni mwao kutilia maanani kina na kumakinikia kwenye kazi inayofanywa. Ujuzi na uwezo zaidi vinajengwa katika masomo ishirini na moja katika mchepuo wa kwanza na wa pili wa Kitabu cha 3, ambayo yamepangiliwa kwenye seti. Kila seti inajumuisha mlolongo wa shughuli zinazomakinikia kwenye moja ya vipengele vya msingi vya Sanaa: mstari, umbo, rangi, mguso, na muundo. Watoto wanaongozwa kutumia kile wanachojifunza kutengeneza taswira na vipande vya kisaa ambavyo huakisi dhima ya masomo—dhima kama vile kutafuta ujuzi, kuishi kwa upatano na wengine, na kuyakita maisha yako katika huduma. Katika njia hii, watoto hujiongezea kina cha uelewa wao wa mawazo yaliyojadiliwa kadri wanavyojipatia ujuzi, stadi na uwezo vinavyohusiana na sanaa za kuona.
Vipengele vya masomo vinasindikizwa na seti ya karatasi za shughuli na, ingawa karatasi haziwezi kutumika kwa kujitenga na masomo yenyewe, yaliyotolewa hapa, ili kwamba zinaweza kupakuliwa na kutengenezwa tena kwa urahisi na walimu kadiri wanavyohitaji.