Maendeleo ya mtaala
Mbinu iliyofuatwa na Taasisi ya Ruhi ya kukuza mtaala siyo kwa kawaida ya kuunda, kujaribu ugani na kutathmini, inayofanywa kwa mtiririko wa mfuatano. Bali hatua ya kwanza katika kuandika seti yoyote ya zana inachukuliwa, pale ambapo tajiriba fulani inapozaliwa kwenye ngazi ya umma katika utekelezaji wa huduma inayoitikia wito wa mahitaji ya maendeleo ya jumuiya moja. Zana hizi huibuka kutokana na tajiriba hii na zinakuwa vielelezo vyake. Kuna, kwa upande mmoja, kumbukumbu ya ujifunzaji ambao hutokea katika kutumia mafundisho ya Imani katika eneo maalum la huduma na, kwa upande mwingine, chombo kwa ajili ya kuweka kiutaratibu ujifunzaji huo. Mbinu imekwisha elezewa katika istilahi zifuatazo katika juzuu ndogo iitwayo Kujifunza Kuhusu Ukuaji:
Katika utekelezaji mbinu ya hapo juu huchukua hali tofauti, kufuatana na asili ya zana inayoendelea kukuzwa. Kwa ujumla, hata hivyo, baadhi ya hatua tatu zinaweza kubainiwa katika mchakato wa ukuzaji, ambao hupelekea kile kinachodhahaniwa kuwa toleo la mwisho lililochapishwa.
Muhtasari wa Mwanzo
Kwenye hatua hii kozi au kitabu hubeba dhana za kimsingi na seti ya aya kutoka maandiko ya Kibahá’í ambayo, yakichukuliwa kwa pamoja, huaminiwa kufanikisha lengo la kielimu linaloongelewa. Kwa kipindi fulani, muhutasari huu wa mwanzo wa mawazo hutumiwa na vikundi vidogo vya watu binafsi ugani, kama sehemu ya juhudi za kuelezea maudhui yenye ufanisi ya kozi.Toleo la kwanza
Kadri utendaji unavyoendelea, zana zinaboreshwa na huanza kuakisi tajiriba mpya iliyopatikana, kuingiza mawazo ambayo yanaibuka kutokana nao. Siyo nadra, kuwa baadhi ya mawazo hurekebishwa, aya mpya za maandiko ya Kibahá’í huongezwa, au mlolongo wa mazoezi rahisi hutambulishwa ili kurahisisha uelewa wa mada au kusaidia kukuza ustadi muhimu au mwelekeo. Kupitia mchakato huu, kozi iliyounganishwa au kitabu huibuka ambacho kwa jumla hujulikana kama “toleo la kwanza”.Toleo la Kabla ya Uchapishaji
Katika wakati inaamuriwa, kwa ujumla juu ya msingi wa hadhi wa maudhui, kuifanya kozi au maandiko kupatikana kwa upana zaidi kama toleo la kabla ya uchapishaji. Kupitia matumizi yake yanayoendelea kutumika, inakuwa dhahiri pale sehemu inahitaji kusogezwa au zoezi moja au lingine linahitaji kurudiwa upya. Matoleo kadhaa yanayofuatana yanaweza kutokea. Pole pole, hata hivyo, marekebisho machache na machache Zaidi yanahitajika kufanikisha kusudi lililokusudiwa la kozi au maandiko, na nyenzo, katika hatua hii, hupelekwa kwa ajili ya kuchapisha.