Elimu ya kiroho kwa ajili ya rika zote
Taasisi ya Ruhi hufanya kozi na programu za kielimu kwa makundi ya umri anuai, kutoka umri mdogo wa 5 au 6 hadi utu uzima. Yaliyotolewa hapo chini ni maelezo ya jitihada zake tatu za hivi karibuni, pamoja na orodha ya nyenzo zinazotumika kwa kila moja. Lazima ieleweke kwamba orodhoa zitaendelea kupata mabadiliko kadri tajiriba ugani inapokua, na majina mapya yataongezwa kadri idadi ya vipengele vya kimtaala vinavyoendelea kukuzwa vifikiapo hatua ambapo vinaweza kusambazwa kwa upana.
Mlolongo mkuu wa kozi, kwa ajili ya wale wenye umri wa miaka 15 na watu wazima
Hapo chini yapo majina ya vitabu vilivyopo kwa sasa katika mlolongo ulioandaliwa na Taasisi ya Ruhi kwa vijana na watu wazima. Vitabu hivi vinakusudiwa kutumika kama mlolongo mkuu wa kozi katika juhudi ya hatua kwa hatua ya kuongeza uwezo wa vijana na watu wazima kuhudumia jumuiya zao. Taasisi ya Ruhi pia ina kuza seti ya kozi zinazochepuka kutoka kitabu cha tatu katika mlolongo kwa ajili ya kuwafunza walimu wa madarasa ya watoto ya Kibahá’í, hali kadhalika seti nyingine kutoka kitabu cha tano kwa ajili ya kuinua wahuishaji wa vikundi vya vijana chipukizi. Hizi, pia, zimeoneshwa katika orodha hapo chini.
Programu ya uwezeshwaji kiroho wa vijana chipukizi
Tangu kuanzishwa kwake, taasisi ya Ruhiimeweka umuhimu maalum kwenye kazi yake na vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 15, hasa, imetafuta kuelewa mienendo ya kudumisha vikundi vidogo katika jumuiya za mahali ambavyo hutoa eneo ambapo vijana wanaweza kujadili mawazo na kuunda utambulisho imara wa kimaadili. Taasisi imegundua majina yaliyoainishwa hapo chini kwa ajili ya kusudi hili. Yamegawanyika katika makundi mawili na yameorodheshwa katika mpangilio wa ugumu.Majina mengine kadhaa hatimaye yataongezwa kwenye programu ya Taasisi kwa ajili ya uwezeshwaji kiroho wa vijana chipukizi.
Majina yote haya yanahusika na maendeleo ya ujuzi wa lugha na nguvu ya kujieleza.Baadhi katika kundi la kwanza pia huelezea dhana za kihisabati na masuala ya kijamii, wakati mengine hutafuta kuandaa vijana kuuendea uchunguzi wa uhalisia wa kimwili, kijamii na kiroho katika namna ya kisayansi. Ingawa dhana za kiroho katika zana za kundi la kwanza zimechotwa kutoka mafundisho ya Kibahá’í, kwa asili siyo za kidini, wala hazishughulikii mada ambazo hasa ni za Kibahá’í. Aina nyingi za mashirika, ikijumuisha taasisi za kielimu, kwa hiyo zitagundua kuwa za kufaa kwa ajili ya programu zao za kielimu kwa vijana chipukizi. Majina ya sasa katika kundi hili ni:
Katika kazi yake yenyewe na vijana, Taasisi ya Ruhi hujumuisha vitu katika kundi la pili, ambalo huwasilisha mada za Kibaha’i. Miongoni mwa mada hizi ni zile ambazo vijana wengi chipukizi mara nyingi husumbuka nazo kama vile, hiari na masaibu na uhusiano tata kati ya hiari na ustadi. Kwa sasa, majina yafuatayo yapo katika kundi hili:
Programu ya uwezeshwaji kiroho inatolewa kwa vijana chipukizi katika makundi madogo, mara nyingi huundwa katika kijiji au ujirani na kijana mkubwa. Taasisi ya Ruhi inaendeleza mlolongo wa kozi za mchepuo, kwa kuanza na Kitabu cha 5 katika mlolongo wake mkuu, kuandaa vijana wakubwa na watu wazima kuhudumia kama “mhuishaji”wa vikundi hivyo. Kama unavutiwa katika kusoma maoni kutoka wale ambao wamekwisha shiriki katika programu, bonyeza hapa.
Madarasa ya Kibahá’í ya watoto kwa ajili ya elimu ya kiroho
Masomo kwa ajili ya madarasa ya watoto ya Kibahá’ì, yanayoanza na Daraja la 1 kwa wale wenye umri wa 5 au 6, yamewasilishwa katika muktadha wa ufunzaji wa mwalimu. Wakati watu kila mahali wana hamu ya kuona watoto wao wakishiriki katika madarasa kwa ajili ya elimu yao ya kiroho, tajiriba imeonesha kwamba changamoto ipo katika mafunzo ya idadi yakutosha ya walimu ili kukidhi hitaji hili. Taasisi ya Ruhi inaendeleza seti za kozi ambazo zinachipua kutoka Kitabu cha 3 kwa ajili ya kuwafunza walimu kuendesha madarasa kwa ajili ya watoto hadi kwenye umri wa miaka 11 au 12. Hapo chini ni kozi ambazo kwa sasa zinapatikana.
Zana zinazohitajika kwa ajili ya madarasa yenyewe yamewasilishwa katika kila kitabu, na sampuli ya masomo na baadhi ya rasilimali zingine zinaweza kupatikana hapa. Hasa wakati wa miaka ya mwanzoni kabisa ya utoto, msisitizo mkubwa unawekwa juu ya maendeleo ya sifa za kiroho na kwenye imani, tabia na ruwaza za mwenendo ambao hujumuisha sifa muhimu za kiumbe wa kiroho.