Kona ya walimu

Watoto wanaohudhuria madarasa ya Kibahá’ì kwa ajili ya elimu yao ya kiroho, yanayofanyika katika jumuiya duniani kote, hutumia muda kujifunza sala kimoyo moyo na aya fupi fupi kutoka maandiko ya Kibahá’í—kama vile “Ni wenye nguvu mno mwanga wa umoja kwamba unaweza kuangazia dunia nzima” na “Hitaji kuu la binadamu ni ushirikiano na kutendeana”. Wanasikiliza hadithi ambazo huwasaidia kuonesha dhana zinazojadiliwa, huimba nyimbo, hucheza michezo yenye ushirikiano, wanajihusisha na tamthilia yenye ubunifu, na kufanya shughuli za kisanii.

Ili kuwasaidia walimu katika kuandaa madarasa, tumekusanya hapa baadhi ya rekodi za nyimbo, halikadhalika maneno ya nyimbo na sauti, ambavyo vinaweza kuimbwa na watoto ili kuleta furaha kwenye mioyo yao na kuimarisha mielekeo ya akili zao na tabia ambazo zitawawezesha kuishi maisha ya furaha na yenye manufaa. Walimu wanaweza pia kupata hapa katika muundo wa PDF karatasi ya rangi na Sanaa kwa ajili ya matumizi ya masomo kwa ajili ya madarasa ya watoto.